14 Juni 2025 - 23:40
Kuangushwa kwa Ndege 10 za Kivita za Utawala wa Kizayuni katika Maeneo Tofauti ya Iran

Kamanda wa Kituo cha Ulinzi wa Anga cha Khatam al-Anbiya(s), ametoa taarifa ya kuangushwa kwa ndege nyingi za kivita za utawala wa Kizayuni.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kamanda wa Kituo cha Ulinzi wa Anga cha Khatam al-Anbiya(s), ametangaza kuwa ndani ya saa moja iliyopita, ndege 10 za kivita za utawala wa Kizayuni zimeangushwa katika maeneo mbalimbali ya Iran.

Aidha, ulinzi wa anga wa mji wa Tehran hivi punde umefanikiwa kuangusha ndege nyingine mbili za kivita katika anga ya mji mkuu huo. Mifumo ya ulinzi wa anga katika miji mbalimbali nchini ikiwemo Dezful pia inaendelea kukabiliana na ndege za kivita za adui Mzayuni.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha